Wednesday, June 29, 2011

CHIEF MPYA WA BUJORA HUYU HAPA

Mwanamuziki Shaggy apishwa kuwa Chief wa kabila la wasukuma Bujora


Mr.LOVER LOVER Mwanamuziki Shaggy kutoka pande za Kingstone Jamaica na marekani akiondoka kwa kucheza huku akiwa ameshikilia usinga na kusindikizwa na vigoli wa kabila la kisukuma wakati alipokuwa akiondoka katika eneo la tukio mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kanbila la wasukuma.

Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani akimshukuru Shaggy mara baada ya kumtawaza kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa.
Shaggy akiwa amekalisha katika kiti cha kichifu cha kisukuma mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa nje kidogo ya jiji la Mwanza, kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo na anayefuata ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndungu.
Hapa naye akikabidhi baadhi ya zana kwa wafayakazi wa Serengeti Breweries baada ya kutawazwa.
Mzee wa kabila la Kisukuma akimkabidhi mkuki mwanamuziki Shaggy wakati alipokuwa akitawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika makumbusho ya Bujora kijiji cha Kisesa.
Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Jaji Mark Bomani akizungumza na mwanamuziki Shaggy kabla ya kutawazwa rasmi.
Wanakijiji wa Kisesa wakicheza moja ya ngoma za kabila la wasukuma.
Chifu Charles Kaphipa akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya kumtawaza mwanamuziki Shaggy, wanaosikiliza kutoka kulia ni Chifu Makwaiya, Allan Chonjo, Caroline Ndungu, Mwanamuziki Shaggy na Mzee Mark Bomani.
Wanakijiji wakiwa wamefurika kwa ajili ya shughuli hiyo kubwa na inayoheshimika sana kwa kabila la wasukuma.
Mwanamuziki Shaggy akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndungu huku wakipepewa kwa nyungo na vigoli wa kabila la wasukuma.
Mwanamuziki Shaggy akisindikiwa na Vigoli wa kabila la Kisukuma wakati akiingia katika uwanja wa ngoma za Bulabo.

Hapa Shaggy akiwa katika jumba linalohifadhi vifaa mbalimbali vya ngoma za wasukuma, kulia ni Padri Fabian Mhoja ambaye ndiyo mhifadhi wa makumbusho ya Bujora (kushoto) ni Jaji Mark Bomani Mwenyekiti wa (SBL)
Shaggy akisalimiana na mzee Pius Ng'wangu wakati alipofika hapo katika makumbusho ya Bujora
Padri Fabian Mhoja ambaye ndiyo mhifadhi wa makumbusho ya Bujora kushoto akimpa mwanamuziki Shaggy maelezo ya makumbusho hayo ya kabila la wasukuma wakati, mwanamuziki huyo alipofika katika makumbusho Bujora na kujionea mambo mbalimbali katika makumbusho hayo, katikati kutoka kushoto ni Jaji Mark Bomani , Caroline Ndungu na Bahati Singh kutoka Serengeti Breweriers.

No comments:

Post a Comment

Tunayaheshimu maoni yako ndio maana tunayahitaji